Skip to main content
Chapati za Maziwa na Mayai.
Mahitaji
- Unga WA Ngano vikombe 8.
- Maji au maziwa au mchanganyiko wa maji na maziwa vikombe 2 na nusu.
- Siagi au margarine (blue band au prestige) vijiko 4 vya kukandia .
- Margarine au siagi ya kukunjia robo kikombe .
- Vanilla kijiko 1 cha chai .
- Hiriki ya unga kijiko
- kimoja cha chai .
- Mafuta ya kukunjia na kuchomea nusu kikombe .
- Unga WA kusukumia kikombe kimoja .
- Chumvi vijiko 3 vya chai .
- Sukari kijiko kimoja na nusu cha chakula .
- Mayai 3.
Jinsi ya kupika .
- Chukua unga wako chekecha kisha weka ndani ya chombo cha kukandia.
- Chukua mayai kisha yapige kwa pembeni.
- Chukua siagi yote kisha yeyusha.
- Weka tobo katikati kisha weka vanilla ,hiriki, Sukari ,Chumvi na mayai yako kisha weka na siagi.
- Kisha changanya kwa Mikono yote 2 huku una sugua sugua.
- kisha vikishachanganyika anza kuweka maziwa au maji au mchanganyiko wa maji na maziwa.
- kisha kanda kidogo Chukua mafuta ya kupikia kijiko 1 cha chai pakaza kwa juu ili donge lako lisiwe kavu na kuweka Ugumu kwa juu.
- kisha funika Kwa saa moja.
- Baada ya saa moja funua kanda tena Kata madonge yako 10 mpaka 13.
- Kisha funika Kama dakika 10.
- Anza kufanya tabaka ( unasukuma chapati yako kisha unapaka margarine au mchanganyiko wa margarine na mafuta kisha una nyunyiza unga unatengeneza tabaka Fanya hivyo kwa zote kisha acha kama dakika 15).
- Bandika chuma cha kuchomea jikoni kikipata moto sukuma chapati yako weka jikoni acha iive geuza upande wa pili acha dakika 1.
- Anza kuweka mafuta pia hadi chapati zako ziive kote kote.
Comments
Post a Comment